Wafanyabiashara ndogondogo almaarufu kama wamachinga katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wameiomba Serikali kupitia Manispaa ya Bukoba kuwatatulia changamoto mbalimbali zinazowakabili katika eneo jipya la machinjio ya zamani ambapo wamehamishiwa kutoka katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na maeneo ya Shaburidini, maeneo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera(Government) maarufu kama Uganda Road pamoja na maeneo tofautitofauti ya Manispaa hiyo ya Bukoba Mkoani Kagera.
Kauli hiyo ilitolewa na baadhi ya wafanyabiashara hizo ambapo ni pamoja na Bi: HUSNA MOHAMED,Respikius Salatieli na mwingine aliye tambulika kwa majina ya Hashimu Mohamedi wote wakiwa wafanyabiashara wa soko hilo jipya la machinjioni barabara ya Kashozi iendayo Migera Katika Manispaa hiyo ya Bukoba .
Wafanyabiashara hao wamesema kuwa changamoto kubwa ambayo inawakabili kwa sasa ni pamoja na kutokuwepo kwa ulinzi wa kutosha katika soko hilo ambapo mali zao walisema kuwa haziko katika usalama, muda wote wanawaza pa kuzipeleka wapi pindi wanapofunga na kuondoka kwenda majumbanikwao ambapo wamesema kuwa ulinzi katika eneo lao hilo unahitajika ili wawe wanaacha biashara zao na kurejea majumbani kwao pasipo kuwa na mashaka yoyote juu ya biashara zao hizo .
Walisema pia Halmashauri ya manispaa hiyo inatakiwa kuwasimamia katika kufanya biashara hiyo kutokana na baadhi ya wamachinga hao kuwa katika vikundi viwili ambavyo ni pamoja na kikundi cha kwanza kushindwa kupanga bidhaa zao ndani ya soko hilo ambapo walipewa eneo na kujenga vibanda lakini cha kushangaza baadhi ya wamachinga wenzao wanashindwa kupanga biashara zao na kuamua kupanga bidhaa hizo mbele kwa kutandaza chini hali ambayo pia wanalalamikiana wao wenyewe katika kile ambacho walisema wanazibiana riziki kw akuwa wateja walio wengi ni wapiti njia na hivyo wanakomea mbele kwa walio tandaza chini na waliomo ndani kushindwa kufikiwa na wateja hao. Hata hivyo Machinga hao walizidi kusisitizakwa kuiomba Serikali kuhakikisha inawaondoa pia wafanyabiashara hao ndogondogo ambao wapo katika maeneo ya stendi Kuu ya mabasi kwa kuwa wameanza kurejea katika maeneo hayo ambayo waliamuliwa kuondoka kwani kuna huduma zingine ambazo zinahitajika katika soko hilo ambapo zinakosekana kutoka na baadhi ya machinga hao kuwa katika eneo hilo la stendi ya mabasi na hivyo kufanya wanunuzi kutoka eneo hilo na kwenda kutafuta eneo jingine na hivyo kuiomba Serikali kulishughulikia suala hilo.
Kadhalika walisema kuwa eneo hilo ambalo wanafanyia biashara hiyo hawana uongozi ambao pengine wangeweza kuwasilisha kero zao na walisema kuwa inakuwa vigumu sana katika kwenda kwa pamoja kuwasilisha matatizo yao katika uongozi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo jambo ambalo pia bado ni changamoto katika kupata hatima ya biashara zao. Hata hivyo Gazeti hili la HAMASA lilifika katika viwanjavya machinga hao mnamo mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Diwani wa kata ya Kahororo ambae pia ni Meya wa Manispaa ya Bukoba Mhe: Chief Kalumuna aliwaambia wamachinga hao kuwa matatizo yao hayo yote ambayo yanawakabili yapo mbioni kutatuliwa na kuwataka machinga hao kuwa wavumilivu pia Serikali ya Mkoa huo wa Kagera kupitia Manispaa hiyo inatambua umuhimu wa wafanyabiashara hao .
Vilevile alipokuwa akiongea nao wamachinga waliweza kumtambulisha uongozi wao mpya walioamua kuuchagua baada ya kuona barua yao ya kuomba uongozi kuchelewa kujibiwa. HAMASA ilifanya mahojiano mafupi na Mwenyekiti aliyechaguliwa na kusema, “Tuliandika barua ya maombi kuhusu uongozi wa soko la machinjioni kwa mtendaji kata Kashai wakaomba tusubiri, baada ya kuchelewa na changamoto kuwa nyingi tukakubaliana kuchagua uongozi wa muda siku ya taehe 25 mwezi huu ambapo mwenyekiti ni mimi Leonidas Kalyamtima, katibu ni Jovonati Clemence na muweka hadhina ni Husna Mohamed” Alimaliza.
Kwa upande wa Meya aliwaambia wamachinga kama wataridhia hao ndo wawe viongozi wao basi wao hawana tatizo, uongozi huo utathibitishwa siku ya kikao rasmi ambacho bado hakijafanyika.
No comments:
Post a Comment