Hivi vitu pichani ni baadhi ni vya kiutamaduni wa Mhaya ambapo vinapatikana Makumbusho ya Kagera (Kagera Museum) |
Kwa Tanzania,kabila la wamasai ndio pekee linalonufaika na Utalii wa utamaduni, ni utalii ambao mtu anaenda sehemu moja kwenda nyingine kujifunza au kuona mambo ya kitamaduni ya jamii husika kama maisha ya watu,ngoma,chakula,mila na desturi,mtalii anaweza kwenda kuona jamii husika kwenye makazi yao au kwenda kwenye nyumba au sehemu zilizohifadhiwa vitu mbalimbali vya kumbukumbu vilivyotumiwa na jamii husika au ambavyo vinaendelea kutumiwa sasa mfano vikapu,mkuki nakadhalika. Kwa nchi zinazoendelea huu utalii umekuwa mpya kwao lakini utalii unatumiwa na nchi zilizoendelea kama Ujerumani,Uingereza na Marekani na unaingizia serikali mapato makubwa.Mkoa uliopakana na nchi nyingi zaidi Tanzania (Mkoa wa Kagera) umejaaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ikiwemo pia utamaduni ambao tukifanikiwa na kuutangaza tutapata wageni wengi sana kuja kuona utamaduni na utaingizia jamii mapato na kupunguza umaskini. Wamasai kutokana na kufanikiwa kuutangaza utamaduni wao,wageni wengi wanaokuja kutembea Tanzania uenda kujifunza na kuwatembeleana kununua vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na wamasai. Familia za kimasai zinanufaika sana na utalii wa kiutamaduni na wanaingiza pesa nyingi sana ,wengine hufanikiwa kuingiza hadi sh. 40,000 kwa siku kutokana na utalii huu wa kiutamaduni.
Utalii wa kiutamaduni una nafasi kubwa sana ya kutoa ajira nyingi na kuingiza kipato kwa mkoa wa Kagera na mikoa mingine ya kanda ya ziwa na kupunguza umaskini uliopo. Mikoa ya kanda ya ziwa imetajwa kwenye ripoti ya serikali kama mikoa duni zaidi japo ina fursa nyingi lakini wananchi wanashindwa kuzitumia sababu ya kukosa elimu.
Mambo ambayo mkoa wa Kagera wanaweza kufanya kutangaza utalii wa kiutamaduni kwanza kutangaza ngoma za asili za makabila mbalimbali yanayopatikana mkoani Kagera,wasanii kama Maua na Saida wamejitaidi sana kutangaza utalii wa ngoma na walifanikiwa kuteka soko la Taanzania na nje ya nchi hivyo inaonesha ni kiasi gani utalii wa kiutamaduni wa mkoa wa Kagera unavyokubalika.
Pili utamaduni wa kumenya ndizi, wageni wengi hasawazungu hawajui jinsi ya kumenya ndizi na huwa wanashangaa mtu anavyoweza kumenya ndizi kwa haraka,kama tukiweza kutangaza utamaduni huu wa kumenya ndizi,wageni wengi watakuja kujifunza kwenye familia mbalimbali namna ya kumenya ndizi na wananchi watanufaika kwa kuongeza kipato na mkoa pia utanufaika.
Tatu mkoa wa Kagera ili kukuza na kutangaza utalii wa kiutamaduni,kila wilaya au mkoa uwe unaandaa siku ya utamaduni na kualika watu mbalimbali kuja kuona utamaduni wa sehemu husika, hii itasaidia kutanga utalii wa kiutamaduni na jamiiitanufaika sana kwa mapato.Wilaya ya Karagwe wamefanikiwa kwa hili kuandaa siku ya utamaduni wa wanyambo na wamefanikiwa kutangaza utalii wao, ni vizuri jitihada zikiendelea za kutangaza utalii huu wa utamaduni.
Nne mkoa wa Kagera ili kutangaza utalii wa utamaduni nashauri watangaze zaidi nyumba au sehemu zinazohifadhi mambo ya utamaduni, kwa muda mrefu kumekuwa nasehemu zinazotunza mambo ya kale lakini kumekuwa hakuna jitihada kubwa kutangaza hizi sehemu. Serikali ya mkoa inaweza kunufaika sana na utalii huu kama jitihada zikiwekwa za kutangaza.Mwisho ili kupunguza umasikini mkoa wa Kagera hatuna budi kutangaza utalii huu wa utamaduni,mkoa umebahatika sana kuwa na vivutio vingi vya asili na utamaduni ikiwemo pia nyumba za asili na historia ya utamaduni wa makabila mbalimbali yanayopatikana mkoa wa Kagera. Ni wakati sasa wa kutumia fursa hizi ili kunufaika nazo na kipato kwa wananchi kiweze kukua.
No comments:
Post a Comment