HAMASA - KAGERA
Senene mdudu anayefanana na panzi ameweza kuwa mdudu wa kuthaminika zaidi katika jamii ya watu wa Mjini Bukoba kwani amekua zao zuri la biashara vilevile ni chakula cha heshima kwa kabila la Wahaya .Wadudu hao(Senene) ni wadudu ambao hupatikana kwa msimu na kwa kiasi kikubwa katika maeneo baadhi ya Mkoa wa Kagera na nje ya mkao wa kagera ambao hutegwa na wengine hukamatwa na watu kwa ajili ya kuliwa nyumbani au kwa ajli ya biashara ni moja kati ya biashara iliyowaingizia wakazi wengi wa Mjini Bukoba kutokana na watu wengi kufurahia chakula ya wadudu hao. Senene hupatikana kwa misimu katika mwezi wa 4 na 11 ambapo huonekana katika maeneo yenye nyasi ndefu au fupi na watu huanzia hapo kuwakamata wadudu hao, watoto kwa wakubwa hujihusisha na kuwakamata Senene kwajili ya chakula au kwajili ya biashara. Wafanyabiashara mbalimbali wamejikita katika biashara ya senene kwasababu imeonekana kuwa nafaida kibiashara. Senene huitajika kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya biashara kila msimu wafanya biashara huwakamata senene kwa wingi katika magunia na madiaba, Ili kukamata senene wengi kiasi hicho huhitajika maandalizi makubwa na ya mda ,Senene kwajili ya biashara hukamatwa jioni au usiku kwa kutumia taa zenye mwanga mkali ambazo hutegeshwa kwajili ya kuvutia senene hao nyakati za usiku pamoja na mabati marefu kwenda juu yaliyoelekezwa kwenye midomo ya madiaba, pia huachiliwa moshi mzito unao vuka kwenda juu ambao ndio humkosesha senene nguvu na kuanguka katika madiaba yaliyo tegeshwa kupitia mabati senene huvutiwa na mwanga nyakati za jioni na huufwata mwanga huo hivyo ndivyo hujikuta wakiliwa.
Zaidi ya asilimia 10.5% ya wakazi wa Mjini Bukoba kila ifikapo msimu wa senene hujikita na biashara hiyo ya Senene na huuzwa kwa mifuko midogo au pakiti au kwa magunia na madiaba kwa fungu la bei ya chini kabisa senene huuzwa shiling 500 pesa ya kitanzania.
Senene ni chakula ya asili ya Muhaya na hupewa heshima kubwa hasa katika maeneo ya vijijini ambako asili hutokea,wagen rasmi katika famili waliokuja kutoa Mahali au Wazee wenye heshima kubwa hukalibishwa kwa kupewa Senene kama heshima ya ujio wa watu hao.
No comments:
Post a Comment