![]() |
Hapa ni eneo la makaribisho'reception' ya Kagera Museum, ambapo kuna vitu mbalimbali vya kiutamaduni wa Mhaya |
NA DIDAS MUGYABUSO
Watanzania wengi ukiwaambia neno Utalii akili yao inahamia Arusha na Kilimanjaro kwenye mbuga ya Serengeti na Mlima Kilimanjaro, kumbe Tanzania kuna vivutio vingi sana, sio hivyo tu. Mfano hapa Kagera tuna vivutio vingi ambavyo vikitangazwa vizuri vinaweza kukuza Uchumi wa Mkoa wetu, vifuatavyo ni baadhi tu;-
Kisima cha Mtagata.
Ni kisima ambacho kina historia kubwa katika utamaduni wa watu wa Kagera na na maajabu ya maji ya kisima hicho ndio hufanya watu wengi kupenda kukitembelea kisima hicho,maji yake ni mazuri kwa tiba kama pumu, matatizo ya ngozi na kuteguka kwa mifupa. Kwa wageni wa ndani na nje uwa wanatembelea sehemu hii kuangalia tiba au uponyaji.
Biharamulo.
Katika Wilaya ya Biharamulo Mkoani kagera unaweza kutembelea maeneo mbalimbali kama Ziwa Burigi, Kisiwa cha Rubondo , German Boma,Bwina peninsula na mazingira Kahugo.
Makumbusho ya Chief Rumanyika.
Makumbusho haya yana historia kubwa ya moja kati ya machifu waliozungumziwa sana katika historia, Makumbusho haya yanapatikana wilaya ya Karagwe,watalii wa ndani na nje hutumia mazingira hayo kwa kutazama historia za kigeni na kitamaduni na kufanyia uchunguzi wa mambo mbalimbali ya kihistoria.
Makumbusho ya Kagera
Yapo maeneo ya Nyamkazi karibu na uwanja wa ndege-Bukoba, masuala yote ya kihistoria ya muhaya utayapata hapa. Vilevile katika Manispaa ya Bukoba unaweza ukatembelea vivutio vingine kama Ziwa Victoria ambapo utakutana na mandhari nzuri ya fukwe za pembezoni mwa ziwa kama Miami beach, Kiroyera beach, Bunena beach, Maruku beach,Paradise beach, Yasira beach, Kalobela beach n.k , vilevile unaweza kufika maeneo ya Ntungamo na kujionea mandhari ya Mji wa Bukoba na Ziwa Victori kwa ukubwa zaidi kutoka juu.
No comments:
Post a Comment