NA JOHNSTONE MWESIGA(MDAU)
Mkoa wetu katika kipindi cha kupatikana uhuru wa Tanganyika baadaye Tanzania tulikuwa kwenye nafasi nzuri sana kiuchumi, lakini miaka ilivyoenda mbele mkoa ukashuka na sasa pato la wakaazi wa mkoa wetu limekuwa ni taabu kweli kweli. Na leo mkoa upo kati ya mikoa mitano iliyoko katika hali mbaya ya umaskini. Hii ni kutokana na tafiti mbalimbali na ni za kweli. Sitapenda kurudia mengi ya wengi wasemayo kuhusu nini kimetufikisha hapa kilammoja anajua na kikubwa ni kutofanya kazi kwa juhudi, mkoa kuwa ‘locked’ hauna mwingiliano watu wengi kutoka nje ya mkoa na nje ya nchi ingawa ndo mkoa unaoongoza kwa kupakana na nchi nyingi. Hii ni kutokana na kutokuwa na fursa wezeshi ambazo zimekwisha kugunduliwa au kubuniwa na sisi wakazi wa mkoa, ili watu wengi kutoka ndani na nje waje kuwekeza kwazo.
NINI KIFANYIKE ILI MKOA UPANDE KIMAENDELEO?
1. KILIMO Mkoa wa kagera
ni moja ya mikoa yenye uhakika wa mvua na vyanzo vya maji kama mito na maziwa ambayo ni support ya mimea ya mazao mengi. Pia matumizi ya mbolea hasa samadi na ile ya viwandani, kutokana na uwepo wa fursa hizo na kwa kuwa kuna hali ya hewa nzuri, ardhi ya kutosha kulima mazao mbalimbali kama matunda, miti, migomba mihogo mbogamboga,mibuni, vanilla na mengne mengi, ila wakazi wa mkoa huu tumekuwa nyuma katika sekta ya kilimo kwa mapana yake. Ambacho kinaweza kutukwamua katika janga la umaskini na kuusogeza mbele kiuchumi kwa mkoa wetu. Hivyo tungewekeza kwenye kilimo chenye tija kwa wakulima, mfano zao kuu letu la biashara kahawa ambalo linastawi karibu katika wilaya zote za mkoa wetu lingefanyiwa mapinduzi halisi kwa kuboresha taasisi zinazosimamia zao hili kuanzia taifa hadi kwenye vyama vya msingi. Tutumie vizuri kituo cha utafiti wa kilimo Maruku, TACRI, KCU, KDCU, ziwe imara kwa ajili ya maslahi ya wakulima na kutoa elimu inayokidhi katika ukulima wa kisasa. Bei ya kahawa iwe yenye kumpa nafuu ya maisha mkulima. Haya si kwa kahawa pekee, iwe pia kwa zao la chai ambalo kiukweli limepoteza mvuto mkoani kwetu, miwa, vanilla,maua, miti ya matunda na mbao iwe na kanuni nzuri za ulimaji na utunzaji. Tuige vyama vingne kama KNCU cha Kilimanjaro,Mbinga coffee growers, nk. Mazao ya chakula pia kilimo chake kiboreshwe tuachane na kulima kimazoea maharage, mahindi, migomba, mihogo, viazi vitamu, mbogamboga hivi vikilimwa kwa ustadi vina soko kubwa. Mfano mhogo unahitajika sana nchi jirani Uganda na Sudan, nadhan huwa tunaona jinsi watu wa Buseresere wanavyouza makopa kule Uganda.Viazi vitamu aina ya karoti ni kirutubisho kizuri kwa afya zetu. hivyo tufanye tafiti na kutumia matokeo ya tafiti hizo kujikwamua katika kilimo
2. UTALII Kagera imejaliwa vivutio vya utalii ambavyo vinaweza kutuingizia pato kama mkoa kupitia makampuni ya kitalii. Vivutio si mpaka vivumbuliwe na wazungu hata sisi tunaweza kugundua maeneo ya vivutio ambavyo ni sehemu ya kuleta watu wenye nia ya kuviona kutoka ndani na nje ya nchi ili tupate pato katika kampuni za kitalii zinazoongoza watalii,pato la mkoa kama kodi, na pato kwa wenye hotel pamoja na wauzaji wa vitu mbalimbali watakvyovutiwa navyo wakiwa matembezini. Kama Sikosei Bukoba yapo makampuni yanayotangaza vivutio vya utalii kama Willy Bukobatours, Kiroyera na Frajo Media, hawa watu wanajitahidi sana katika kuendeleza utalii Kagera. Ila tuwaunge mkono tuendelee kubainisha maeneo mengine mfano kuna kisiwa kilichopo ziwa Victoria kati ya Kemondo na Bukoba karibu na mwambao wa Maruku.Kinaweza kuwa kivutio kikifanyiwa utafiti kuona kuna aina gani ya wanyama na mimea, ndege au kama hakuna ni wanyama gan waletwe ili kukidhi haja ya utalii.Maporomoko ya mito, chemi chemi, kuendeleza miambao ya maziwa,mapango n.k
3. MICHEZO Michezo ni moja ya sekta muhimu katika kuleta mandeleo ya kiuchumi sehemu husika,michezo inakutanisha watu mbali mbali ,inaboresha mahusiano baina ya watu, michezo inajenga afya kwa wachezaji pia inawapatia wanajamii kipato kuptia kutoa huduma wakati wa michezo au kushiriki katika michezo husika. Mkoa wetu ni mmoja ya mikoa ambayo iko katika kiwango fulani cha michezo si kizuri au si kibaya sana ila juhudi zinahitajika kuimarisha maana kijumla michezo hatuishabikiisana. Mpira wa miguu tushukuru tuna timu ligi kuu, ila bado tuweze kuwa nazo zaidi ya moja itakuwa vizuri, tumshukuru malinzi na TFF kwa uboreshaji wa uwanja wa kaitaba. Ila bado tuhitaji kuwa na viwanja vingne vingi kwa mkoa mzima kwa michezo mbalimbali, netball, basketball, volleyball, n.k ili tuweze kuvuutia waandaji wa michezo mbali mbali kuandaa michezo yao mkoani kwetu mbali na kwenda kila mwaka Dar es salaam. Tushukuru pia Misenyi kuna kiwanja cha gofu. Kuanzisha matamasha mbalimbali yenye tija mfano mbio za marathoni mfano Lweu, Marathon, Kagera Marathon au jina lingne lolote lenye mvuto. Hii ni kwa kutafuta wadhamini mfano viwanda vilivyoko Kagera vikadhamini, Kagera sugar, Tanica, Yetuchai, viwanda vya maji na soda na juice vikaweka mkono kudhamini huku vikitangaza bidhaa zake, hata vituo vya redio vilivyoko mkoani takriban vitano vikapewa fursa hiyo....
4. AFYA NA MAZINGIRA
Miji yote ya Kagera haina mpangilio maalumu na usafi wake wa mazingira hauridhishi,hivyo tuwekeze katika kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira uboreshaji wa miundo mbinu ya maji, barabara, stend zetu, upandajimiti, usafi wa kila mara, nyumbani na mtaani, ili ile hali ya hewa nzuri ya Kagera ionekane katika usafi wa mazingira, pia katika afya zikiboreshwa hospitali zetu na kujengwa nyingne kubwa kama ya kansa na ya watu wa orthodox inaweza kuletamabadiliko makubwa pia katika uchumi wamkoa wetu. Kikubwa ni serikali na wadau kuwapa nafasi wawekezaji na kuhakikisha huduma hizi zinakuwepo.
5.VIWANDA-Tunavyo viwanda vikubwa na vidogo hapa sina mengi maana viwanda vya Kagera sijuimaafisa masoko wake wanajua kufanya kazi? Wajitahid kutafuta masoko ya nje nakuboresha brand6.
6.ELIMU- Kila mmoja wetu anaelewa juu ya neno NSHOMILE neno hili lilikuwa na maana sana, kwani jamii yetu ilienda shule awali kuliko wakazi wa mikoa mingine, na kutokana na hilo tulitegemea ELIMU ikawe nuru kwa mkoa wetu. Lakini leo neno nshomile limegeuka kama kebehi kwa watu wa Kagera. Ukilisikia tu unatamani kuficha uso, na wameshatujua watu wa nje ya Kagera wanatukejeli kweli kweli. Hebu tujiulize tuna vyuo vya serikali vingapi katika mkoa wetu ukilinganisha na mikoa mingine. Kuna vyuo vya kati ukiachana na vyuo vikuu, mfano chuo cha kodi,chuo cha maendeleo ya jamii, chuo cha Ustawi wa Jamii, Nyuki, Maji, Ardhi, FTC,Uhasibu na vingne vingi, hivi sijui ilikuwa mpango wa kuiondoa Kagera kwenye ramani ya wasomi maana utasikia vyuo vingi nilivyovitaja ni kigoma, Iringa,Arusha, Kili, Mbeya, Mtwara, Singida, Tabora ndo usiseme, Mwanza Mara, n.k. Ila Kagera ni Kagemu na Katoke. Kwa vyuo vikuu upande wa serikali utasikia wanaplan kuanzisha chuo mara, Katavi Arusha, n.k si KAGERA.Haya yote sawa lakini je sisi tumejipangaje kuwasomesha watoto wetu na sisi ili turudi kama zamani kuondoa aibu hii inayotutafuna?
Maoni ya Mdau:
JOHNSTONE MWESIGA
No comments:
Post a Comment