![]() |
Pichani: Majengo Warriors (Jezi Nyekundu) Vs Ibosa FC (Jezi ya Bluu) |
Ni katika michuano ya Kombe la Ng’ombe lililodhaminiwa na
mtu aliyetajwa kwa jina moja ‘Amri’, ambapo michuano inatarajia kwisha mwishoni
mwa mwezi wa 9, jumla ya timu zinazoshiriki ni 9, na sasa wapo kwenye hatua za mwisho.
Mshindi wa kwanza atapewa dhawadi ya ng’ombe ‘aliyenona’, wa pili ataibukia na
kitita cha shilingi laki 2, na wa tatu laki 1. Pichani ni timu za Majengo
Warriors na Ibosa FC zikitoana jasho katika uwanja wa shule ya Ibosa, ambapo
walitoka sare kwa kufungana bao 1-1, mfungaji wa Ibosa ni Ramadhan Yusuph
(Kapirima) na Majengo Warriors ilifungiwa na Fikiri David kupitia faulo ya
kiufundi.
No comments:
Post a Comment