Friday, September 23, 2016

POLISI YASAMBARATISHA MKUTANO WA UKAWA KAGERA


Polisi yasema hakuna taarifa za mkutano huo, yawataka kufuata waathiriwa majumbani.
Akizungumza na watu takribani sabini waliokuwa wamesubiri viongozi na wageni taifa kuwasili mjini Bukoba katika viwanja vya shule ya msingi Kashai, afisa upelelezi wa polisi wilaya ya Bukoba, amesema kuwa wameshatoa maelekezo kuwa wafanye mkutano wa ndani, na kama ni kuzungumza na waathiriwa wa tetemeko, wanatakiwa kuwazungukia kwenye maeneo yao.
Awali, Mh. Wilifred Muganyizi Lwakatare, aliwaalika wananchi kuudhuria mkutano huo, wakiwasihi kumuunga mkono kuuliza maswali kwa mwakilishi wa mkuu wa wilaya ambaye angejifika mkutanoni hapo.

Tuesday, September 20, 2016

Wimbo mpya wa Diamond 'kumfufua' Saida Karoli?


Tangu ulipotoka wimbo wa Salome alioufanya Diamond akitumia vionjo vya wimbo uliofanya vizuri sana ndani na nje ya nchi wa Saida Karoli 'Chambua kama karanga' watu wengi wamekuwa wakihoji kuhusu makubaliano baina ya watu hao wawili yakoje. Haya ndio majibu aliyoyatoa Diamond;-


Diamond amesema kuwa mwanamuziki huyo mkongwe wa nyimbo za asili ana asilimia 25 kwenye pesa ambazo wimbo huo utakuwa unaingiza,

“Kitu tulichokifanya kabla ya kurealise wimbo,tulizungumza na uongozi wake tukawaambia tunafanya ichi,ichi na ichi, kuna kiasi pia tukakitoaili kiende kwake alafu tukampa 25 percent ya publishing kila income ya publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa anapata percent” Diamond ameiambia Perfect 255.

Saida Karoli alipata mafanikio makubwa kupitia wimbo huo ikiwa ni pamoja na kutumika kwenye filamu ya muandaji maarufu wa Hollywood, Tyler Perry.

Shindano la kisura wa gazeti la Hamasa laendelea kupamba moto

Warembo waliojitokeza kwenye Toleo la pili la gazeti la Hamasa wakijinadi, kama unataka kushiriki bado hujachelewa, wasiliana nasi sasa tukupe utaratibu ili tuweze kukujumuisha kwenye toleo la 3 la Gazeti hili

Taarifa ya TUSHIRIKISHANE kwenye gazeti la HAMASA

Muonekano wake kabla gazeti halijawa printed


Mbunge wa Bukoba Mjini (katikati), Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media kwa pamoja wakisaini 'MoU
'

 Semina ikiendelea


Washiriki wa semina katika Picha ya pamoja



Hii ni taarifa rasmi iliyochapishwa kwenye Toleo la Pili la Gazeti la Hamasa
Jamii Media, waendeshaji wa mtandao maarufu kwa JamiiForums walikuwa mjini Bukoba kwa siku tatu mfululizo kuanzia Tarehe 3 hadi 5 Agosti, 2016 kwa ziara maalum ya uzinduzi wa Mradi uitwao Tushirikishane.
Mradi huo ambao upo katika hatua ya majaribio una malengo ya kuwasaidia viongozi wa kuchaguliwa na wananchi hususani wabunge kutekeleza ahadi walizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita kwa urahisi. Pia mfumo shirikishi unaotumika katika kuendesha Mradi wa Tushirikishane utasaidia Halmashauri kuboresha na kutoa huduma za jamii kwa ufanisi zaidi.
Akiongea mbele la Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media na Mwanzilishi-Mwenza wa mtandao wa JamiiForums, Ndg. Maxence Melo aliwashukuru viongozi wa Manispaa ya Bukoba, Madiwani na Mbunge Jimbo la Bukoba Mjini kwa kuupokea mradi wa Tushirikishane na kuonyesha utayari wa hali ya juu katika kushiriki utekelezaji wake.
Aliongeza kuwa, Tushirikishane itatekelezwa katika Majimbo Sita(6) na Jimbo la Bukoba Mjini limekuwa la kwanza kuingia katika hatua ya utekelezaji.
Naye Mbunge wa Bukoba Mjini, Mh. Wilfred Lwakatare alizisifu jitihada za Jamii Media katika kuchochea uwajibikaji hususani kwenye sekta ya umma nchini Tanzania. Aliupongeza ubunifu na dhima iliyomo ndani ya mradi wa Tushirikishane na kuyafananisha maudhui yake na nadharia ya “Usimamizi Lazimishi”
Katika warsha hii, washiriki walikuwa ni kutoka makundi yanayowakilisha wadau wakuu wa mradi; ambayo ni wananchi/wapigakura, viongozi wa kuchaguliwa na uongozi wa Halmashauri wamepata kujua malengo, muundo wa mradi, wajibu wa wadau na jinsi ya kushiriki katika hatua na shughuli mbalimbali za mradi. Pamoja na shughuli hizo, yako matukio mengine makuu mawili yalitendekeka sambamba na warsha hii katika kuelekea kwenye utekelezaji wa mradi.
Washiriki walipata kupitia ahadi zilizotolewa na mgombea aliyeshinda kiti cha Ubunge, jimbo la Bukoba Mjini na kuchagua ahadi kuu tatu kwa umuhimu zinazoweza kutekelezeka ndani ya miezi tisa toka sasa.
Ahadi zilizochaguliwa ni fungu la kwanza linajumuhisha Ujenzi wa Kituo cha Mabasi Kyakailabwa, ujenzi wa Soko-Kuu la Bukoba na soko la Kashai, namba mbili ni kuwawezesha vijana na akinamama kujiajiri kwa kuwapa mikopo ya riba nafuu na mwisho ni kurasimisha makazi na maeneo mapya.
Pamoja na vipaumbele hivi, Mh. Lwakatare na Madiwani walikubaliana kuwahamasisha wakazi wa Jimbo la Bukoba Mjini kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya. Suala hili limekubalika kuwa mtambuka na hivyo litakuwa mada ya kudumu katika mikutano ya hadhara na ziara za viongozi.
Warsha ya Tushirikishane ilienda mbali zaidi kwa kuandaaa Mpango-Kazi wa utekelezaji wa ahadi zilizochaguliwa kutekelezwa chini ya usimamizi wa mradi. Ili kuhakikisha pande zote zinazohusika katika Mradi zinatekeleza makubaliano, randama (Memorandum of Understanding) ilisainiwa kati ya Ndugu Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media ambaye atatambulika kama msimamizi na muendeshaji wa mradi, Mh. Wilfred Lwakatare Mbunge Jimbo la Bukoba Mjini - mhusika mkuu katika utekelezaji wa ahadi, na Mstahiki Meya, Chief Karumuna kwa niaba ya Baraza la Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ambalo lina jukumu la kuhakikisha huduma za jamii na Sheria ndogondogo zinaboreshwa.
Jamii Media pia ilimtangaza Mhadhiri Happiness Essau na kumuwezesha kwa kumpatia vitendea kazi vitakachomuwezesha kufanya kazi za Afisa Mawasiliano wa Mradi katika Jimbo la Bukoba Mjini kwa ufanisi. Mhadhiri Happiness atakuwa na jukumu la kukusanya na kusambaza habari zilizothibitishwa juu ya maendeleo ya utekelezaji wa Mpango-Kazi.
Njia zitakazotumika kupashana habari ni pamoja na mitandao ya kiganjani (WhatsApp, Telegram), uzi maalumu kwenye tovuti ya JamiiForums.com, makala kupitia FikraPevu.com, kurasa za mitandao ya Twitter, Facebook, Instagram zinazomilikiwa na Jamii Media na kupitia vyombo vingine vya habari.
Gazeti lako pendwa la HAMASA ni mdau aliyeidhinishwa kutoa taarifa rasmi juu ya maendeleo ya mradi wa Tushirikishane kwa Jimbo la Bukoba Mjini. Wananchi na wadau wenye kiu ya kuiona Bukoba ikipiga hatua kimaendeleo wanakaribishwa kuitumia HAMASA kuonyesha jinsi gani Tushirikishane inaweza kupanuliwa kwa faida kubwa zaidi.
Description: https://ssl.gstatic.com/ui/v1/icons/mail/images/cleardot.gif



- MWISHO -

KOMBE LA NG’OMBE KUENDELEA KUTIMUA VUMBI




Pichani: Majengo Warriors (Jezi Nyekundu) Vs Ibosa FC (Jezi ya Bluu)



Ni katika michuano ya Kombe la Ng’ombe lililodhaminiwa na mtu aliyetajwa kwa jina moja ‘Amri’, ambapo michuano inatarajia kwisha mwishoni mwa mwezi wa 9, jumla ya timu zinazoshiriki ni 9, na sasa wapo kwenye hatua za mwisho. Mshindi wa kwanza atapewa dhawadi ya ng’ombe ‘aliyenona’, wa pili ataibukia na kitita cha shilingi laki 2, na wa tatu laki 1. Pichani ni timu za Majengo Warriors na Ibosa FC zikitoana jasho katika uwanja wa shule ya Ibosa, ambapo walitoka sare kwa kufungana bao 1-1, mfungaji wa Ibosa ni Ramadhan Yusuph (Kapirima) na Majengo Warriors ilifungiwa na Fikiri David kupitia faulo ya kiufundi.

Fahamu vivutio vya Utalii Kagera

Unavifahamu vivutio vya Utalii Kagera?


Hapa ni eneo la makaribisho'reception' ya Kagera Museum, ambapo kuna vitu mbalimbali vya kiutamaduni wa Mhaya



NA DIDAS MUGYABUSO

Watanzania wengi ukiwaambia neno Utalii akili yao inahamia Arusha na Kilimanjaro kwenye mbuga ya Serengeti na Mlima Kilimanjaro, kumbe Tanzania kuna vivutio vingi sana, sio hivyo tu. Mfano hapa Kagera tuna vivutio vingi ambavyo vikitangazwa vizuri vinaweza kukuza Uchumi wa Mkoa wetu, vifuatavyo ni baadhi tu;-


Kisima cha Mtagata.
Ni kisima ambacho kina historia kubwa katika utamaduni wa watu wa Kagera na  na maajabu ya maji ya kisima hicho ndio hufanya watu wengi kupenda kukitembelea kisima hicho,maji yake ni mazuri kwa tiba kama  pumu, matatizo ya ngozi  na kuteguka kwa mifupa. Kwa wageni wa ndani na nje  uwa wanatembelea sehemu hii kuangalia tiba au uponyaji.

Biharamulo.
Katika Wilaya ya Biharamulo Mkoani kagera unaweza kutembelea maeneo mbalimbali kama Ziwa Burigi, Kisiwa cha Rubondo , German Boma,Bwina peninsula na mazingira Kahugo.

Makumbusho ya Chief Rumanyika.
Makumbusho haya yana historia kubwa ya moja kati ya machifu waliozungumziwa sana katika historia, Makumbusho haya yanapatikana  wilaya ya  Karagwe,watalii wa ndani na nje hutumia mazingira hayo kwa kutazama historia za kigeni na kitamaduni na kufanyia uchunguzi wa mambo mbalimbali ya kihistoria.

Makumbusho ya Kagera
Yapo maeneo ya Nyamkazi karibu na uwanja wa ndege-Bukoba, masuala yote ya kihistoria ya muhaya utayapata hapa. Vilevile katika Manispaa ya Bukoba unaweza ukatembelea vivutio vingine kama Ziwa Victoria ambapo utakutana na mandhari nzuri ya fukwe za pembezoni mwa ziwa kama Miami beach, Kiroyera beach, Bunena beach, Maruku beach,Paradise beach, Yasira beach, Kalobela beach n.k , vilevile unaweza kufika maeneo ya Ntungamo na kujionea mandhari ya Mji wa Bukoba na Ziwa Victori kwa ukubwa zaidi kutoka juu.

Tajirika kupitia Ufugaji wa Nyuki kwa mtindo wa kisasa




NA FRANK JOHNSON

Kufuga nyuki na kuzalisha asali kwa mtindo wa kisasa kwa kujenga nyumba ya nyuki inamwezesha mfugaji wa nyuki kuongeza uzalishaji wa asali na hatimaye kupata kipato zaidi.Ufugaji wa nyuki ni kazi ambayo imekuwepo kwa karne nyingi sana.Shughuli ya ufugaji wa nyuki nchini Tanzania hasa katika mkoa wa Tabora ambao ni maarufu kwa uzalishaji wa asali ilianza kutambulika rasmi tangu mwaka 1884, wakoloni kama Rebman na craft walipofika katika eneo hilo. Kwa kutambua faida za ufugaji wa nyuki, Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu  Salum Kijuu aliweza kukabidhi mizinga ya nyuki kwa vijana na kina mama wa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera ili iwasaidie kufanya kazi hiyo kwa ufanisi  na kuweza kujipatia kipato kizuri. Hivyo kwa kutambua umuhimu wa ufugaji wa nyuki,Gazeti la Hamasa limeamua kutoa elimu hii kwa wafugaji wa nyuki ili waweze kufuga kwa mtindo wa kisasa na kuweza kabisa kuondoa umaskini kwa vijana kupitia ufugaji huu.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UFUGAJI WA NYUKI.

NYUMBA YA NYUKI.
Hii ni aina mpya ya ufugaji wa nyuki ambapo unaweza kujenga kibanda au nyumba kisha kuweka mizinga idadi unayohitaji.

SABABU YA KUJENGA NYUMBA AU KIBANDA.
• Ni muhimu kufuga nyuki kwenye kibanda kwa sababu inasaidia kudhibiti wizi wa mizinga pamoja na wanyama wanaokula asali.
• Inarahisisha utunzaji wa mizinga na kuwafanya nyuki wasihame kwenda sehemu nyingine.
• Inasaidia watu wengi kujifunza namna nzuri ya ufugaji wa nyuki, ikiwa ni pamoja na watoto jambo ambalo linafanya shughuli hii kuwa endelevu.
• Uzalishaji unaongezeka, hii ni kwa sababu mizinga inayotumika ni ile ya kibiashara.mzinga 1 unapata asali kilo 30 sawa na lita 20.
• Ufugaji wa aina hii usaidia kuwakinga nyuki dhidi ya majanga kama vile moto na mafuriko.
• Inawaepusha nyuki na usumbufu unaoweza kuwafanya nyuki wasizalishe kwa kiwango kinachotakiwa

AINA YA NYUMBAUnaweza kujenga nyumba yenye upana wa futi 3 na urefu wa futi 9.Nyumba hii inaweza kuchukua mizinga 50, halikadhalika unaweza kujenga kibanda chenye ukubwa sawa na huo.

ENEO LINALOFAA.

• Ili kuwa na ufanisi mzuri,nyumba hii inafaa kujengwa nje kidogo ya makazi ya watu
• Kusiwe na mifugo
• Iwe sehemu ambayo watoto hawawezi kufika
• Isiwe karibu na njia ambayo watu wanapita mara kwa mara
• Kusiwe na aina ya mimea ambayo nyuki hawapendi.na kuwe na maji karibu.

MAVUNO
Baada ya kujenga nyumba, kuweka mizinga na nyuki kuingia, unaweza kuvuna kwa mara ya kwanza baada ya miezi mitatu (3).Utaweza kupata mavuno mazuri endapo utavuna kabla nyuki na wadudu wengine hawajaanza kula asali.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa wadudu waharibifu kama vile sisimizi, mende na wengineo wanadhibitiwa ili kutokuathiri uzalishaji wa asali.
Hakikisha unavuna kitaalamu UMUHIMU WA ASALI.

• Asali inatumika kama chakula
• Asali inatumika kama tiba ya magonjwa mbalimbali.
• Asali hutumika kutibu majeraha.
• Ni chanzo kizuri cha mapato.
• Hutumika kutengeneza dawa za binadamu.
• Asali inaweza kuhifadhiwa kwa miaka mingi sana bila kuharibika.Hii inatokana na wingi wa dawa maalumu iliyonayo inayofanya isiharibike

BIDHAA ZITOKANAZO NA ASALI.
• Asali yenyewe.
• Royal Jelly: Hii ni aina ya maziwa

yanayotengenezwa na nyuki ambayo hutumika kama tiba

.• Gundi: Hii hutumika kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya mtumiaji.

• Nta: Hutumika kutengeneza mishumaa kulainisha nyuzi, kutengeneza dawa ya viatu, mafuta ya kupaka, pamoja na dawa ya ngozi.

Hivo kuna soko kubwa sana la asali kutokana na mahitaji yake, ni jukumu lako mjasiriamali kuwekeza kwenye kufuga nyuki. Mnaweza mkawa kikundi na hatimaye mkashirikiana kufuga nyuki kwa ajili ya kupata asali ili kujikwamua kiuchumi.


MISS KAGERA



Anaitwa Bhoke Maria Tubeti, ni Mrembo anayeshikilia taji la ulimbwende Mkoa wa Kagera, na pia aliweza kuingia 5 bora Miss Lake Zone. HAMASA tulipiga naye stori mbili tatu kutaka kujua maisha yake ya umiss kwa ujumla.Tuliongea naye mambo mengi, kwa ufupi hizi ndizo nukuu muhimu kutoka kwake.
NINI KILIMVUTIA KUSHIRIKI UMISS?
“Tokea niko mtoto napenda mambo ya urembo,ili niweze kutimiza ndoto zangu niliamua kushiriki umiss”
“Napenda kuwa Mwanamitindo wa kimataifa, biashara za urembo, Mungu akijalianitafungua bonge la Saloon Mwanza”
CHANGAMOTO
“Kila kitu unajigharamia mwenyewe na vitu ni expensive, matumiz yanazidi hata zawadi  unayopata”
“Mambo ya kishirikina mkiwa kambini”
ALIA   NA WAANDAAJI
“wandaaji wengi ni waswahili sana, wanataja zawadi na fursa nyingi ila mwisho wa siku hakuna lolote,  kwa mfano mimi  bado sijamaliziwahela yangu ya Miss Lake Zone ila nikapotezea”
“ Kuna haja ya kubadili waandaji na kuwapa watu wengine nafasi ili tupate mabadiliko kwa sababu unakuta muandaji  anaandaa zaidi  ya miaka kumi, lazima atarudia makosa tu”.

Ngeze: Nshomile gani hawasomi Vitabu?

Mzee Pius Ngeze akifanya mahojiano na HamasaTalkshow


NA DIDAS MUGYABUSO

Mzee Pius Ngeze ambaye ni nguli wa siasa nchi, na ameweza kushika nyadhifa kubwa mbalimbali nchini ikiwa pamoja na Ubunge ameongea na HAMASA na kusema baada ya kustaafu siasa aliamua kujikita na kipaji chake cha uandishi, ambapo anamiliki kampuni yake ya uchapishaji wa vitabu iliyopo mjini Bukoba inayoitwa Tanzania Educational Publishers (TEPU). Alisema aliingia kwenye uandishi kwa vile una mchango mkubwa kwani neno lililoandikwa halifutiki milele, na kitabu ni urithi, yeye atakufa lakini vitabu vitabaki ,aliendelea kusema, “watu wengi hawaoni umuhimu wa vitabu, lakini ipo siku wataona umuhimu huo na watavisoma”. Akijibu swali la mwandishi alisema anaandika kukidhi haja, anapoona mahali kuna pengo anapenda alizibe kupitia uandishi huo. Lakini kabla ya kuandika ni lazima afanye utafiti kwenye vyanzo mbalimbali kwani vitabu vyake vingi ni vya kisayansi. Umahiri wake wa kuandika vitabu vya kuelimisha hasa kwenye upande wa kilimo ulimfanya apate tuzo kadhaa kama kutambua mchango wake.
“Ninapenda zaidi kuandika upande wa kilimo kwa kuwa nina digrii ya kitu hicho hivyo anaandika kitu nachokijua, lakini pia si mvivu wa kusoma, naendelea kusoma kila sikuili nipate elimu zaidi”. aliongeza. Soko lake kubwa la vitabu ni Halmashauri za wilaya, na vinasambazwa Tanzania nzima na  nje ya Tanzania. Aidha aliongelea  vitabu alivyowahi kuandika vikapendwa zaidi ambavyo ni ‘Misingi ya kilimo bora’ kilichotoka mwaka 1975 ambacho anasema kinauzika hadi leo, pia kitabu cha ‘Ufugaji wa kuku’, anasema kinauzika sana kila kona Tanzania, na kitabu kingine kinaitwa ‘Silaha 100 za kiongozi’. Aliiambia HAMASA  kuandika kitabu sio lazima uwe na digrii, mtu yeyote anaweza kuandika, kwani Shaban Robert kaandika vitabu vingi vinavyotumika hadi leo pamoja na kwamba hana digrii. Pia vitabu vyake vinalenga zaidiwatu wa vijijini ,  wakulima, wafugaji na wavuvi hivyo teknolojia haijaathiri mauzo ya vitabu, kwani kwa vijijini sio watu wengi wenye smartphone au Tv. Kabla hajamaliza mazungumzo alituachia ‘dongo’ lenye ukweli wana Kagera, “watu wa hapa ‘wahaya’ wanajiita Nshomile, Nshomile gani hawasomi vitabu?” Alihitimisha kwa kusema kuwa  elimu lazima iwepo ya kuhamasisha watu kupenda kusoma tangia wadogo, sio vitabu vya darasani tu kwa ajili ya kushinda mtihani, vitabu vya hadithi mbalimbali pia kwani vinajenga, kwani  usomaji wa vitabu ni chakula cha ubongo, inamuongezea uwezo wa kufikiri na kujenga hoja nyingi na zenye maana Kubwa sana katika maisha ya kawaida ya mwanadamu.

MAONI YA MDAU: MAENDELEO HAYALETWI NA MAKONGAMANO

Mkoa wa Kagera ni mojawapo ya mikoa kongwe kabisa hapa Tanzania. Hapo mwanzo ulijulikana kwa jina la Mkoa wa Ziwa Magharibi kumaanisha ni mkoa ulio karibu na Ziwa Victoria. Mkoa huu umejaaliwa kila aina ya neema na rasilimali. Kilimo cha ndizi na kahawa ndiyo mazao makuu kwa ajili ya uchumi wa wanaKagera. Kwa upande mwingine mkoa huu umejaaliwa shughuli za uvuvi unaoendelea katika ziwa victoria ambapo  kuna uvuvi mkubwa samaki aina ya sangara, sato na dagaa. Mbali na rasilimali zote hizi kuna watu mashuhuri ambao wametokea katika mkoa huu ambao wamechangia Maendeleo makubwa katika mikoa mingine. Lakini kumetokea changamoto kubwa ya kimaendeleo kiasi kwamba mkoa huu umetajwa kati ya mikoa maskini zaidi hapa Tanzania. Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango alitoa takwimu hizi wakati akiwasilisha taarifa ya tathimini  ya mwaka 2015/2016 alionesha kuwa mkoa huu una umaskini wa asilimia 39.3 wilaya ya Biharamulo inaongoza kwa umaskini zaidi. Takwimu zinaonesha kuwa wakazi wa mkoa huu wana kipato cha chini kabisa na shughuli za uzalishaji haziwaingizii kipato kama inavyostahili kulinganisha na mikoa mingine. Takwimu ya wizara ya fedha inaonesha kuwa asilimia kubwa ya wakaazi wa mkoa huu mbali na kipato cha kila mtanzania kimepanda kutoka shilingi 770,464 mwaka 2010 hadi  shilingi 1,919,928 kwa mwakabado kipato hiki hakijafikiwa na watanzania wengi wa mkoa huu. Hatuwezi kuzibeza wala kuzidharau takwimu hizi kwani zina maana kubwa kwa maisha ya kila siku ya wanaKagera. Na katika kujadili umaskini ni lazima kuweka mapendekezo ya nini kifanyike ili kukinusuru kizazi cha mkoa huu ambao una historia kubwa kwa Maendeleo ya taifa hili.
Kilimo na ufugaji, huu ni utimgongo wa watanzania wengi lakini katika mkoa huu wakulima wengi hawalimi kwa ajili ya biashara bali hulima kwa ajili ya kula tu (subsistence) ambapo inakuwa ngumu kwao kushindana na uzalishaji wa mikoa mingine. Kilimo cha mkoa huu kimekuwa cha mazoea sana kiasi kwamba wakulima hawajibadilisha fikra zao na namna ya uendeshwaji wa kilimo. Zao la ndizi ambalo limetegemewa kwa karne nyingi limekumbana na ugonjwa wa mnyauko(Banana Xanthomonas wilt) ambapo uzalishaji wa ndizi umepungua kwa kasi sana. Kilimo kinapaswa kubadilishwa kwa wakulima kulima mazao mbadala kama viazi, ufuta,mihogo na mazao ambayo sio ya msimu. Aidha kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu kwa wananchi kujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji. Mkoa huu umejaaliwa mito na mabwawa pamoja na maziwa kadhaa ambayo yanaweza kuwa chanzo cha maji. Mwambao wa Mto Ngono ni mojawapo ya eneo lenye rutuba kubwa kinacho hitajika ni kuweka utaratibu wa vikundi kwenda kuanzisha kilimo cha mazao ambayoyanaweza kuwa ya chakula na biashara pia. Kilimo cha umwagiliaji kinaweza kutatua tatizo la chakula hapa mkoani. Biashara, sekta ya biashara ni moja wapo ya sekta ambayo ina manufaa makubwa sana mkoa huu una bahati ya kuwa mpakani na nchi za Rwanda, Burundi, Uganda ambazo zinaweza kuwa chanzo kikubwa cha mahusiano ya kibiashara kwa wakazi wa mkoa huu. Mipaka inapaswa kutumika kama kitovu cha uchumi wa mkoa huu, kuna bidhaa ambazo hazipatikani katika mataifa jirani ambazo wananchi wakihamasishwa wakasafirisha mpaka huko wanaweza kupata masoko pamoja na mahusioano mema ya kibiashara. Lakini pia biashara ya ndani kwa ndani ni mojawapo ya kitu muhimu kwa wananchi pamoja na uchumi wa mkoa mzima. Biashara zote kubwa na ndogo zinapaswa kuwekewa utaratibu mzuri ambao utawanufaisha wafanyabiashara na wananchi. Pia uwekezaji kwenye bidhaa za chakula nafaka pamoja na biashara ambazo zinaendana na kasi ya karne hii. Wadau wa Maendeleo, mkoa huu una watu mbali mbali ambao wameendelea kiuchumi lakini hawajaweza kujiwekeza katika mkoa huu ili  kuwanufaisha wakaazi wa mkoa huu.Aidha juhudi za wadau hawa kamwe hazitoshi, kumekuwa na makongamano pamoja na vikao vya wadau wa Maendeleo wa mkoa huu ambavyo havijazaa matunda kwani ushirikiano unakuwa ni mdogo au ushirikiano na walengwa unakuwa ni mdogo sana. Kwa upande mwingine Maendeleohayawezi kuletwa na watu waliopo mbali ila ni juhudi za watu waliomo ndani ya mkoa kwani waliopo nje huweza kuja wakiona kuwa waliopo ndani wametia nia na juhudi za kujikwamua kimaendeleo.
Uvuvi, sekta ya uvuvi ni mojawapo ya maeneo ambayo yanaweza kulikuza pato la mkoa huu. Kuna maziwa kama Ikimba,Burigi, Victoria pamoja na mito mikubwa ambayo ipo mkoani kama Kagera na Mto Ngono. Lakini kwa takwimu zilizopo ni kwamba samaki wengi wanaotumiwa Rwanda wanasafirishwa kutoka Mwanza jambo ambalo linapaswa kubaki aibu kwa wafanyabiashara na wavuvi wa mkoa wa Kagera. Sio kwamba samaki hawapo ila tatizo ni mfumo wa uvuvi pamoja na mawazo ya wavuvi. Mfano takwimu zinaonesha kuwa kipato cha uvuvi kimeshuka kutoka tani kilo 150 kwa mtumbwi hadi kilo 15 kwa mtumbwi. Njia za uvuvi zinazotumika bado ni za kiasili na wavuvi wengi wamelenga soko la ndani tu. Kilimo cha uvuvi kinapaswa kuimarishwa sana kwa kuhamasisha uvuvi wa kisasa na kuweka misingi ambayo mazao ya uvuvi yatapata soko la ndani na nje.
Kwa upande mwingine mkoa huu una vivutio kadhaa vya utalii ambavyo vikitangazwa  vyema vitakuwa chachu ya kuwaleta watalii na kuinua biashara za mahoteli pamoja na kuutangaza utamaduni wa mkoa wa Kagera. Utamaduni wa ngoma, mavazi chakula vikitumiwa kisawa sawa ni jambo muhimusana katika kuukuza utalii na mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi. Maendeleo ni mojawapo ya kilio cha watanzania wengi, kuna umuhimu mkubwa wa wakazi wa mkoa huu waliopo ndani na nje kuweka na kutekeleza mipango mikubwa kwa ajili ya kuinua kipato chao. Juhudi za serikali pekee hazitoshi kuinua kipato na kuondoa umaskini. Mikoa mingi ambayo imeendelea haijaendelea kwa sababu ya juhudi za serikali ila ni juhudi za wananchi pekee na serikali inakuwa chanzo cha kuweka utaratibu ili mwananchi wanufaike.
 Pia nguvu kazi ambayo ni vijana inapaswa itumike kisawa sawa kwani inaonekana kuwa vijana wengi siku hizi wanakimbilia mijini na kufanya kazi ambazo zinaingiza kipato kwa muda mfupi. Hii hurudisha nyuma uzalishaji wa mazao na chakula. Vijana kama nguvu kazi inapaswa wawe watu wa kwanza kabisa katika mchakato wa kuleta Maendeleo kwa jamii. Vijana wakiwa katika vikundi au mmoja mmoja wawekewe utaratibu mzuri ambao watatumia fursa zilizopo kwa kila mkoa kwa manufaa ya vizazi vijavyo pamoja na kizazi hiki. Pia Maendeleo hayawezi kuletwa kwa vikao na makongamano bali kuna umuhim mkubwa wa kutekelea miradi na mipango ya Maendeleo kwa ajili ya manufaa ya wanaKagera.

Maoni ya WEKISHA K KARUMNA (Mwanafunzi wa UDSM na Mkazi wa Muleba)

Mdau: Je Kagera inaweza kuondoka katika umaskini wa kipato?

NA JOHNSTONE MWESIGA(MDAU)

Mkoa   wetu   katika   kipindi   cha   kupatikana   uhuru   wa   Tanganyika   baadaye   Tanzania tulikuwa   kwenye   nafasi   nzuri   sana   kiuchumi,   lakini   miaka   ilivyoenda   mbele   mkoa ukashuka na sasa pato la wakaazi wa mkoa wetu limekuwa ni taabu kweli kweli. Na leo mkoa upo kati ya mikoa mitano iliyoko katika hali mbaya ya umaskini. Hii ni kutokana na tafiti mbalimbali na ni za kweli. Sitapenda   kurudia   mengi   ya   wengi   wasemayo   kuhusu   nini   kimetufikisha   hapa   kilammoja  anajua   na kikubwa  ni   kutofanya  kazi  kwa  juhudi,   mkoa   kuwa  ‘locked’   hauna mwingiliano   watu   wengi   kutoka   nje   ya   mkoa   na nje   ya   nchi   ingawa   ndo   mkoa unaoongoza   kwa   kupakana   na   nchi   nyingi.   Hii   ni   kutokana   na   kutokuwa   na  fursa wezeshi ambazo zimekwisha kugunduliwa au kubuniwa na sisi wakazi wa mkoa, ili watu wengi kutoka ndani na nje waje kuwekeza kwazo.

NINI KIFANYIKE ILI MKOA UPANDE KIMAENDELEO?
1. KILIMO Mkoa wa kagera

ni moja ya mikoa yenye uhakika wa mvua na vyanzo vya maji kama mito   na   maziwa   ambayo   ni   support   ya   mimea   ya   mazao   mengi.  Pia   matumizi   ya mbolea hasa samadi na ile ya viwandani, kutokana na uwepo wa fursa hizo na kwa kuwa kuna hali ya hewa nzuri,   ardhi ya kutosha kulima mazao mbalimbali kama matunda, miti, migomba mihogo mbogamboga,mibuni, vanilla na mengne mengi, ila wakazi wa mkoa huu tumekuwa nyuma katika sekta ya kilimo kwa mapana yake.  Ambacho kinaweza kutukwamua katika janga  la umaskini na kuusogeza mbele kiuchumi kwa mkoa wetu. Hivyo tungewekeza kwenye kilimo chenye tija kwa wakulima, mfano zao kuu letu la biashara   kahawa   ambalo   linastawi   karibu   katika   wilaya   zote   za   mkoa   wetu lingefanyiwa mapinduzi halisi kwa kuboresha taasisi zinazosimamia zao hili kuanzia taifa hadi kwenye vyama vya msingi. Tutumie vizuri kituo cha utafiti wa kilimo Maruku, TACRI,   KCU,   KDCU,   ziwe   imara   kwa   ajili   ya   maslahi   ya   wakulima   na   kutoa   elimu inayokidhi katika ukulima wa kisasa. Bei ya kahawa iwe yenye kumpa nafuu ya maisha mkulima.   Haya   si   kwa kahawa   pekee,   iwe   pia   kwa   zao   la   chai   ambalo   kiukweli limepoteza mvuto mkoani kwetu, miwa, vanilla,maua,  miti ya matunda na mbao iwe na kanuni nzuri  za  ulimaji na utunzaji.  Tuige  vyama vingne kama KNCU cha  Kilimanjaro,Mbinga coffee growers, nk.   Mazao   ya   chakula   pia   kilimo   chake   kiboreshwe   tuachane   na   kulima   kimazoea maharage, mahindi, migomba, mihogo, viazi vitamu, mbogamboga hivi vikilimwa kwa ustadi vina soko kubwa. Mfano mhogo unahitajika sana nchi jirani Uganda na Sudan, nadhan huwa  tunaona jinsi  watu wa Buseresere wanavyouza makopa  kule Uganda.Viazi vitamu aina ya karoti ni kirutubisho kizuri kwa afya zetu.   hivyo tufanye tafiti na kutumia matokeo ya tafiti hizo kujikwamua katika kilimo

 2. UTALII  Kagera imejaliwa vivutio vya utalii ambavyo vinaweza kutuingizia pato kama mkoa kupitia makampuni ya kitalii. Vivutio si mpaka vivumbuliwe na wazungu hata sisi tunaweza kugundua maeneo ya vivutio ambavyo ni sehemu ya kuleta watu wenye nia ya kuviona kutoka ndani na nje ya nchi ili tupate pato katika kampuni za kitalii zinazoongoza watalii,pato   la   mkoa   kama   kodi,   na   pato   kwa   wenye   hotel   pamoja   na   wauzaji   wa   vitu mbalimbali watakvyovutiwa navyo wakiwa matembezini. Kama Sikosei Bukoba yapo makampuni yanayotangaza vivutio vya utalii kama  Willy Bukobatours,  Kiroyera  na  Frajo Media, hawa watu  wanajitahidi sana katika kuendeleza utalii Kagera. Ila tuwaunge mkono tuendelee kubainisha maeneo mengine mfano kuna kisiwa kilichopo ziwa Victoria kati ya Kemondo na Bukoba karibu na mwambao wa Maruku.Kinaweza kuwa kivutio kikifanyiwa utafiti kuona kuna aina gani ya wanyama na mimea,   ndege   au   kama   hakuna   ni   wanyama   gan   waletwe   ili   kukidhi   haja   ya   utalii.Maporomoko   ya   mito,   chemi   chemi,   kuendeleza   miambao   ya   maziwa,mapango n.k

3. MICHEZO Michezo ni moja ya sekta muhimu katika kuleta mandeleo ya kiuchumi sehemu husika,michezo inakutanisha watu mbali mbali ,inaboresha mahusiano baina ya watu, michezo inajenga   afya   kwa   wachezaji  pia   inawapatia   wanajamii   kipato  kuptia   kutoa   huduma wakati wa michezo au kushiriki katika michezo husika. Mkoa wetu ni mmoja ya mikoa ambayo iko katika kiwango fulani cha michezo si kizuri au si kibaya sana ila juhudi zinahitajika kuimarisha maana kijumla michezo hatuishabikiisana. Mpira wa miguu tushukuru tuna timu ligi kuu, ila bado tuweze kuwa nazo zaidi ya moja itakuwa vizuri, tumshukuru malinzi na TFF kwa uboreshaji wa uwanja wa kaitaba. Ila   bado   tuhitaji   kuwa   na   viwanja   vingne   vingi   kwa   mkoa   mzima   kwa   michezo mbalimbali, netball, basketball, volleyball, n.k ili tuweze kuvuutia waandaji wa michezo mbali mbali kuandaa michezo yao mkoani kwetu mbali na kwenda kila mwaka Dar es salaam. Tushukuru pia Misenyi kuna kiwanja cha gofu. Kuanzisha matamasha  mbalimbali yenye tija mfano mbio za marathoni mfano Lweu, Marathon,   Kagera   Marathon   au   jina   lingne   lolote   lenye   mvuto.   Hii   ni   kwa   kutafuta wadhamini mfano viwanda vilivyoko  Kagera vikadhamini, Kagera sugar,  Tanica,  Yetuchai, viwanda vya maji na soda na juice vikaweka mkono kudhamini huku vikitangaza bidhaa zake, hata vituo vya redio vilivyoko mkoani takriban vitano vikapewa fursa hiyo....

4. AFYA NA MAZINGIRA
Miji yote ya Kagera haina mpangilio maalumu na usafi wake wa mazingira hauridhishi,hivyo tuwekeze katika kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira uboreshaji wa miundo mbinu ya maji, barabara, stend zetu, upandajimiti, usafi wa kila mara, nyumbani na mtaani, ili ile hali ya hewa nzuri ya Kagera ionekane katika usafi wa mazingira, pia katika afya zikiboreshwa hospitali zetu na kujengwa nyingne kubwa kama ya kansa na ya watu wa orthodox inaweza  kuletamabadiliko makubwa pia katika uchumi wamkoa wetu. Kikubwa ni serikali na wadau kuwapa nafasi wawekezaji na kuhakikisha huduma hizi zinakuwepo.
5.VIWANDA-Tunavyo viwanda vikubwa na vidogo hapa sina mengi maana viwanda vya Kagera sijuimaafisa  masoko  wake wanajua  kufanya  kazi?  Wajitahid  kutafuta masoko ya  nje  nakuboresha brand6.
6.ELIMU- Kila mmoja wetu anaelewa juu ya neno NSHOMILE neno hili lilikuwa na maana sana, kwani jamii yetu ilienda shule awali kuliko wakazi wa mikoa mingine, na kutokana na hilo  tulitegemea   ELIMU  ikawe   nuru   kwa   mkoa   wetu.  Lakini   leo   neno  nshomile limegeuka kama kebehi kwa watu wa Kagera. Ukilisikia tu unatamani kuficha uso, na wameshatujua watu wa nje ya Kagera wanatukejeli kweli kweli. Hebu tujiulize tuna vyuo vya serikali vingapi katika mkoa wetu ukilinganisha na mikoa mingine. Kuna vyuo vya kati ukiachana na vyuo vikuu, mfano chuo cha kodi,chuo cha maendeleo ya jamii, chuo cha Ustawi wa Jamii, Nyuki, Maji, Ardhi, FTC,Uhasibu   na   vingne   vingi,   hivi  sijui   ilikuwa mpango   wa   kuiondoa   Kagera kwenye   ramani   ya   wasomi   maana   utasikia   vyuo   vingi   nilivyovitaja   ni   kigoma, Iringa,Arusha, Kili, Mbeya, Mtwara, Singida, Tabora ndo usiseme, Mwanza Mara, n.k. Ila Kagera ni Kagemu na Katoke. Kwa vyuo vikuu upande wa serikali utasikia wanaplan kuanzisha chuo mara, Katavi Arusha, n.k si KAGERA.Haya yote sawa lakini je sisi tumejipangaje kuwasomesha watoto wetu na sisi ili turudi kama zamani kuondoa aibu hii inayotutafuna?

Maoni ya Mdau:
JOHNSTONE MWESIGA

Historia ya Karagwe kuandikwa upya

Akizungumza na Hamasa mwanzilishi wa siku ya Utamaduni wa Wanyambo ‘alifunguka’  kama ifuatavyo;-

MUANDAAJI - Kazi hii ya kuunda upya historia ya karagwe  lilikuwa wazo la watu wawili ambao ni mimi mwenyewe, Bullet Straton Ruhinda (Sociologist/ Anthropologist) na Edward Frontline Ruhinda (Environmental Engineer). Wazo lilikuwa ni kuandika historia hii kwa kutumia mbinu yaani kutumia mtazamo kwa namna ya kuwapitia wazee na watu wote wenye historia ya Karagwe ili kuweza kuiweka kwenye kumbukumbu kwa kizazi kijacho”. Pia ababu ya wazo hili ilikuwa ni kwamba Karagwe inayo historia kongwe sana hapa Tanzania ukiondoa historia ya ukanda wa Pwani hasa Zanzibar na Kilwa, Karagwe ilifuata kwa ukongwe. Pia Karagwe ni moja kati ya falme  katikaAfrika ya Mashariki hasa  kwa Tanzania..Historia ya Karagwe ukiondoa Prof Katoke na Mzee Pesha, imeandikwa zaidi na wageni wakiaongozwa na Speke, Prof. Birgita Farelius na wengineo. Katika kuikusanya historia hii kulikuwa na mpango wakufanya utamaduni wa Karagwe na Kagera kwa ujumla kuwa chanzo cha utalii. Hii ni pamoja kufufua makumbusho kama Ikulu za Karagwe na kuzifanya kuwa vivutio vya watalii.Vilevile kulikuwepo mpango wa kuzitambua na kuzikusanya mali za kale za karagwe na kuzihifadhi vizuri kwa kizazi kijacho. Baadhi ya mali za kale hizo zipo mikononi mwa watu na nyingine zipo serikalini ila utunzaji wake sio mzuri. Zipo sehemu kama Mtagata, na maeneo ya maziko ya Bakama ambayo yameanza kuharibika yanatakiwa kutunzwa na kuhifadhiwa na bado Kuna mchakato wa kushirikiana na serikali na wadau wengine ambapo tuliona ni vema kuanzisha siku ya utamaduni ambayo itakuwa inaazimishwa kila tarehe 21 Mei ya kila mwaka na huu ni mwaka wa pili mfululizo kuanzia mwaka 2015. Tarehe hiyo kila mwaka kunakuwa na maonyesho ya kitamaduni  na mali za kale toka maeneo mbalimbali ya Karagwe. Kwa kweli mwitikio ni mzuri sana kama  nitakumbuka vizuri mwaka jana watu walisafiri toka Karagwe nzima kuja kuazimisha siku ya tarehe 21 Mei. Mwaka huu imekuwa na ufanisi mkubwa zaidi, watu wamesafiri toka mikoani kuja kushuhudia.. Pia mwaka huu kulikuwa na wawakilishi kutoka nje ya nchi. Ufalme wa Bunyoro  pia falme jirani kama Kianja(Kamachumu), Busubi(Biharamulo) na Bugufi(Ngara). Wote hao wamekuja kwa gharama zao.
Katika harakati zetu tumejaribu kupitia falme za zamani kuangalia jinsi ya kuifanya historia ya Kagera iwe katika nyaraka. Baadhi ya falme tumepitia ni pamoja na Kianja, Kyamutwara na Bugufi.

Aliendelea kwa kusema kuzungumzumzia upande wa uwezeshaji wa Tamasha ambapo alisema, “Kwa asilimia kubwa naliwezesha mimi, wananchi wanachangia kidogo, kwa upande wa Serikali imesaidia sana katika kuweka mazingira ya kufanyika kwa Tamasha”.
Aidha ametoa shukrani kwa Redio za kijamii kama Fadeco na Karagwe kwa mchango wao wa matangazo ya bure kuhusu Tamasha hilo.walipendekeza baadae iwe ya kimkoa. Ndio maana tulifikia hatua ya kwenda katika Falme nyingine kama Bugufi, Kianja na Busubi. Mwakani tamasha linategemea kuhusisha watu wengi zaidi toka mkoani Kagera maana Kagera ni moja na utamaduni unakaribiana sana.


"Nina nyimbo zaidi ya 90"- Nshomile

Israel Didas(Nshomile Family), msanii wa nyimbo za asili Bukoba




NA HAMASA
Nshomile Family sio jina geni kwa wakazi wa  Mkoa wa Kagera, ni kundi lililopata kutamba Mkoani humo kutokana na kazi mbalimbali walizozifanya. Kundi hilo linaundwa na wasanii wawili Israel Didas na Ras Voice. Gazeti hili la HAMASA Lilipiga  stori na Israel Didas ambaye ni memba wa kundi hilo, alisema mziki alianza rasmi mwaka 2008, ana album moja sasa,  msanii huyo wa miondoko ya Afropop Alisema mziki alianza kufanya akiwa shule ya msingi baada ya kugundua kipaji chake, kabla ya kuingia studio alikuwa akifanya show mbalimbali za jukwaani zikiwemo show za kampeni ambapo zilimuwezesha kujilipia mwenyewe studio. Wimbo uliomtambulisha katika game ni Ondeke (Uniache) alioufanyia studio ya Mwanza inayoitwa Kivuli
“Mwanzo nilianza kwa kuimba nyimbo za kawaida kwa Lugha ya Kiswahili, baadaye nikaamua niwe natumia kihaya kwenye nyimbo zangu baada ya kugundua nakubalika zaidi upande huo wa nyimbo za asili” Aliendelea. Akijibu swali la mwandishi anasema si lazima msanii wa Kagera aimbe kihaya ndio atoke, kwani wasanii kama BK Sunday na Shemela walitambulika kwa kuimba nyimbo za Kiswahili kabla hawajabadilika na kujikita kwenye kihaya.
Aliendelea kusema kuwa kwa sasa amekuwa hasikiki sana kutokana na matatizo ya kifamilia, hata hivyo ana nyimbo mpya ambazo zinaendelea  kuchezwa na vituo mbalimbali vya redio na tv, nyimbo hizo ni Ndo Hao na Kajakaro. Anaamini  kwa Tanzania msanii hawezi kufanikiwa kwa kiasi kikubwa bila kwenda Dar ambapo kuna  media na studio kubwa, hivyo akipata mtu wa kumuwezesha na kusimamia kazi zake atafanya hivyo kwani ana nyimbo nyingi sana.
“Nina nyimbo zaidi ya 90 ambazo bado hazijarekodiwa”, aliongeza.

Mafanikio aliyopata kwenye mziki ni kujulikana na pia unamuwezesha kujikimu kimaisha, kwani hupata mialiko sehemu mbalimbali kama kwenye, maharusi, mijuburo, matamasha mbalimbali , n.k. 
Kuhusu sanaa ya  Mkoa wa Kagera kwa sasa anasema haina mwelekeo, ni kama wasanii wametelekezwa, kwani hakuna watu wa kusimamia kazi zao kama ilivyokuwa huko nyuma enzi za kina Saida Karoli ambao walitamba na nyimbo mbalimbali kama chambua kama karanga. Msanii wa Mkoa wa Kagera anae mkubali kwa sasa ni Sarah wa Kakau Band, na msanii chipukizi anayemkubali ni Molly P ambapo alisema kuwa  anamshukuru Mungu kwani mashabiki wamekuwa wakizipokea vizuri sana kazi zake, kitu kinachomkwamisha ni wadau wa kumuwezesha ili aweze kusonga mbele zaidi. Alisema kuwa  anaupenda sana mziki na anahisi bado anaudai, na anawapenda sana mashabiki zake, vilevile amewaomba waendelee kuwasapoti wasanii wa nyumbani wanaofanya vizuri.

Kagera Movie kimataifa

NA HAMASA

Baada ya kushuhudia Filamu mbalimbali zilizoigizwa na wasanii mbalimbali kutoka Mjini Bukoba Mkoa wa Kagera sasa waigizaji hao wamejipanga kutoa Filamu itakayoweza kuuzwa kimataifa, tukiongea na mtunzi wa stori ya Filamu hiyo muigizaji nguli kutoka Bukoba na mmiliki wa Tuzo ya Filamu bora Kanda ya Ziwa Victoria, Onyango Ochola ambaye amekwisha tengeneza Filamu mbalimbali Mjini  Bukoba kama Kaburi la Mama na nyingine nyingi, muigizaji huyo mwenye muda mrefu akifanya  sanaa ya Filamu  alizungumzia Filamu hiyo ya Safari Ya Mauti itakua ni moja kati ya kazi kubwa za Filamu alizowahi kufanya maana amejipanga na ni Filamu yenye ubora na viwango vya hali ya juu akilinganisha na zile alizowahi kufanya. Movie hiyo ya Safari Ya Mauti ameizungumzia kama Filamu iliyolenga sana maswala ya kijamii na inayotoa maelekezo katika jamii ili kuenenda katika maadili yanayofaa. Alisema ni Filamu itakayohusisha mazingira mbalimbali nchini Tanzania yakihusisha pia mazingira ya Mkoa wa Kagera pamoja na maeneo mengine nchini Tanzania , Filamu hiyo ni mojakati ya Filamu kubwa za Mji wa Bukoba zilizoshirikisha mastaa mbalimbali wa nchini Tanzania wanao fanya vizuri katika sanaa ya Maigizo, wasanii hao ni kama Hashimu kambi na Dude ,mbali na Filamu hiyo kushirikisha mastaa hao pia imewahusisha waigizaji mbalimbali kutoka Mjini Bukoba ambao pia ni washiriki wa Filamu hiyo, alizungumzia namna alivyo wahusisha wasanii hao kutoka Mjini Bukoba alisema ilimbidi afanye usaili wa kuangalia vipaji vya Kuigiza kwa watu mbalimbali ili kupata washiriki hao katika Filamu hiyo ya Safari Ya Mauti. Usahili huo uliofanyika viwanja vya Linaz Night Club Mjini Bukoba siku ya 25-27/05/2016 ndio uliomuwezesha kupata Wasanii wa kuchezeshwa katika Filamu  hiyo kutoka Mjini Bukoba pia mbali na kupata wasanii hao ilimlazimu awafanyishe mazoezi ili waweze kuiva zaidi katika Filamu hiyo na kufanya vizuri. Aliwaomba wapenzi mbalimbali wa Filamu kuunga mkono juhudi hizo katika Filamu hiyo ili sanaa hiyo  iweze kufika  mbali.

Msanii na mtayarishaji wa Filamu Kagera bwana Onyango Ochola

Maua arudi kivingine




NA HAMASA

Mmoja kati ya wanamuziki wakongwe na mahiri mkoani Kagera Maua Chenkula akizungumza na HAMASA alizungumzia ujio wake mpya katika gemu la muziki wa asili vilevile soko la muziki wa asili Mkoa wa Kagera na Tanzania kwa  ujumla, hiki ndicho alicho kisema “Nawaomba  mashabiki  zangu waelewe kwamba sijaacha  Muziki ila nilisimama kutokana na matatizo,hata hivyo mwaka juzi nimetoa Albamu iitwayo TINKILYA ina nyimbo saba(7) zikiwa ni audio,vilevile mwaka jana nikazitolea video nyimbo zote saba (7) na kwa sasa nimetoa wimbo mpya unaitwa ENGONZI MILEMBE na tayari nimeutengenezea video ambayo itatoka muda wowote.Albamu yangu ya TINKILYA  inanyimbo saba ambazo ni Tinkilya, Kazoni, Tanzania, Ninsiima, Bandeke, Bakundekele na Nsheshe.” Msanii mkongwe wa nyimbo za asili aliongezea kwa kuainisha malengo yake katika Albamu yake ya TINKILYA, “Katika Albamu hii ya TINKILYAninamalengo ya kuendeleza muziki wa asili yetu ili usipotee na kuutangaza ndani na nje ya Tanzania ili waujue , kuitangaza Tanzania na mimi mwenyewe kujipatia kipato kupitia  albamu hiyo.”
Maua Chenkula ambaye aliuza sana kazi zake za nyimbo za asili kipindi cha miaka ya nyuma alizungumzia mabadiliko katika soko la muziki wa nyimbo za asili kwa kipindi hiki alisema,”Mabadiliko ni makubwa sana katika faida ya muziki wa asili mfano, zamani muziki wa asili ulikuwa hauna kipato ulikuwa unaburudisha na kuelimisha tu,laikini kwa sasa muziki wa asili unaelimisha pia unakupatia kipato.Muziki wa asili wa sasa umekuwa na thamani na jamii imeutambua kuwa ni kazi ,nami nawahakikishia kuwa muziki ni kazi kama kazi nyingine na unakipato kizuri.” Akiwa anamalizia mazungumzo yake na Gazeti  la Hamasa Mwanamuziki Maua Chenkula ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya TMMT 2015-16 kama Muimbaji bora wa kike wa nyimbo za asili zilizotolewa Mjini Bukoba aliizungumzia tuzo hiyona kwa namna ilivyo muhamasisha katika kazi zake ,”Tuzo niliyopata niliifurahia sana na ilinihamasisha kuendeleza muziki wa asili maana niliona kuwa watu wananikubali Maua kama Maua  ndo maana walinichagua kuwa mshindi nawashukuru  sana mashabiki wangu na wapenzi wote wa nyimbo za asili kwa kunipa moyo  na ninawaahidi  wategemee mambo mazuri sana maana tayari nimejipanga  sawasawa na ninajua wimbo wangu mpya wa ENGONZI MILEMBE (Yaani upendo ni Aman) wataupenda una meseji nzuri sana na umetengenezwa ki utaalamu zaidi.”


Oddy Paisy akizungumzia muziki wa Bukoba




Odetha Pais 'Oddy Pais' katika pozi


NA HAMASA
Msanii wa nyimbo za Asili na Zuku anayetamba Mjini Bukoba na Vijijini kwa wimbo wake wa asili wa “Taa Rutha” alizungumzia Muziki wa Bukoba na sababu zinazokwamisha  mzikihuo kufika mbali na kutoa wasanii wakubwa zaidi wa kuiwakilisha Bendera ya Tanzania kutoka Bukoba zaidi ya walivyofanya  Saida Karoli, Bk-Sande na wengine wengi. Akizungumza na gazeti la Hamasa msanii huyo wa muziki Odetha Pais maarufu kama Oddy Pais alisema, “Mziki wa Bukoba umepiga hatua kwa kiasi fulani mpaka sasa tofauti na ulivyokua mwanzo enzi za Saida Kaloli,Maua Chenkula na Revina Kasabira kwani kwa sasa wapo wanamuziki wengi Mjini Bukoba wanajihusisha na muziki vilevile wamejituma kutengeneza video zilizo  na ubora zaidi  na miondoko ya muziki wa asili ya Mjini Bukoba  imebadilika sana”.Mwanamuziki huyo Odi Pais anayeandaa matamasha yake mwenyewe na huwashirikisha wasanii mbalimbali wa mbalimbali ndio njia inayomtangaza msanii Mjini Bukobakama  B-Friends na wengine wengi alizungumza kuwa , “Njia ya kuimba katika  majukwaa na
matamasha kwa kiasi kikubwa katika jamii na ndio njia inayomuingizia fedha msanii maana kwa Tanzania hakuna mikakati mingine mizuri ya kumuingizia msanii wa muziki fedha tofauti na kuimba katika matamasha mbalimbali yanayo andaliwa”.
 Aliendelea kusema “Bado mwamko wa wanaKagera ni mgumu, watu hawapendi kukubali vitu vyao na hushobokea  vitu vya nje, hivyo hutupa wakati mgumu wasanii katika kazi zetu au waandaaji wa matamasha kwani ukiandaa tamasha  la wanamuziki wa Bukoba tu inakua ngumu kupata washabiki labda awemo na staa katika tamasha hilo, hivyo washabiki wa mziki waache mazoea na kukariri na wafwatilie vipaji vipya vilivyomo mjini mwao”.
 Akimalizia mahojiano yake na Gazeti la Hamasa msanii huyo aliwaomba mashabiki wa muziki wajiandae kwa kazi zake nzuri zaidi anazo ziandaa.

Monday, September 19, 2016

"Tetemeko halijaletwa na Serikali"-Rais Magufuli




Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na tetemoko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera na mikoa jirani ya Mwanza, Geita na Mara kutoka kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Ikulu DSM.

Pamoja na kupokea taarifa hiyo Rais Magufuli amepokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki mbili (USD-200,000/-) sawa na takribani Shilingi za Kitanzania Milioni Mia nne na therathini na saba (Tshs-437,000,000/-) kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni na pia amepokea taarifa ya mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

Katika taarifa yake Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema tetemeko hilo limesababisha vifo vya watu 17, majeruhi 440, nyumba 2063 zimeanguka, nyumba 14,081 zipo katika hali hatarishi na nyumba 9,471 zimepata uharibifu mdogo, huku watu 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

Mhe. Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali zikiwemo kupeleka chakula, huduma za matibabu na hifadhi za dharura kwa waathirika na pia inaratibu ukusanyaji wa michango kutoka sehemu mbalimbali ambapo mpaka sasa kiasi cha Shilingi za Kitanzania Bilioni tatu nukta sita (Tshs Bilioni 3.6) zimepatikana.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya maafa na michango kwa ajili ya waathirika wa maafa hayo, Rais Magufuli amewashukuru wote waliojitoa kusaidia waathirika wakiwemo Marais Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Mhe. Uhuru Kenyatta wa Kenya na Paul Kagame wa Rwanda ambao wamempigia simu za kumpa pole na tayari wametoa misaada yao, na pia nchi mbalimbali, mashirika, wafanyabiashara, watumishi wa umma na watu binafsi na amesema michango hiyo ina umuhimu mkubwa katika kukabiliana na athari za maafa haya.

Dkt. Magufuli ametoa wito kwa Watanzania na wote walioguswa na maafa haya kuendelea kutoa misaada kwa waathirika kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, huku akionya na kuvitaka vyombo vya dola kuwafuatilia watu wanaotaka kutumia maafa haya kukusanya michango kwa lengo la kujinufaisha.

Rais Magufuli amebainisha kuwa Serikali itahakikisha inarekebisha miundombinu iliyoharibika zikiwemo shule, vituo vya matibabu, barabara na huduma nyingine za kijamii na pia ametaka wananchi waliokumbwa na madhara ya tetemeko hususani nyumba zilizobomoka, wajipange kurekebisha nyumba zao kwa kuwa Serikali pekee yake haitaweza kujenga nyumba zote zilizobomoka.

Aidha, Rais Magufuli amewasihi Watanzania kuwapuuza watu wanaotaka kutumia maafa haya kueneza uchonganishi na chuki dhidi ya Serikali na ameweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna teknolojia ya kutabiri kutokea kwa tetemeko la ardhi na kwamba tetemeko hili halikuletwa na Serikali.

Dkt. Magufuli amesema hata mataifa makubwa yenye maendeleo makubwa ya uchumi na teknolojia yanakumbwa na tetemeko la ardhi na kusababisha vifo vya idadi kubwa ya wananchi na uharibifu mkubwa wa mali.

"Nilikuwa najaribu kuangalia kwa mfano nchi kama China kwenye mwaka 2014 watu 617 walipoteza maisha, Mwaka 2013 walipoteza watu 193, Mwaka 2010 walipoteza watu 2,998 Mwaka 2008 China ilipoteza watu 98,712.

Ukijaribu kuangalia Japan, nchi ambayo imeendelea na ina utaalamu wa hali ya juu sana, kwenye mwaka 2016 tarehe 14 mwezi wa nne ilipoteza watu 6, baada ya siku mbili tarehe 16 mwezi wa nne 2016 tetemeko likatokea tena na likaua watu 35, mwaka 2012 likaua watu 3, mwaka 2011 likaua watu 15,904 mwaka 2008 likaua watu 12, mwaka 2007 likaua watu 11, mwaka 2004 likaua watu 40, mwaka 1923 liliua watu 142,800 na hiyo ni Japan. Amesisitiza Rais Magufuli.

Shughuli ya kupokea taarifa ya Waziri Mkuu na michango kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera na Mikoa jirani imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Suzan Kolimba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mhe. Dorothy Hyuha na Naibu Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Boniface Muhia.




Chanzo: IPP Media

Grey Muclass

Grey_Hapana Official Video Directed by Owokusiima

Sam Master Ft. OCBaby

Video ya msanii na producer kutoka Bukoba





Ally de Young Venom

Video ya msanii wa Rap kutoka Bukoba mjini



Amuah Real

Video ya msanii Amuah Real kutoka Bukoba




'Wille Kiroyela'

Mkurugenzi wa Bukoba Cross Culture Travel & Tours, Ndugu William Oswald Rutta ambaye pia ni diwani wa kata ya Ishozi akiongelea shughuli zake za utalii na siasa...


Vision FM CEO

Mahojiano na Valerian, mmiliki wa Vision Fm kwenye kipindi cha Hamasa TalkShow



Mzee Pius Ngeze

Mahojiano na mzee Pius Ngeze kwenye kipindi cha Hamasa TalkShow

Diamond ametukumbushia wahaya

This Song was written by Diamond Platnumz & Rayvanny in Tanzania 2016 from Originally Song Maria Salome by Saida Karoli... The beat was produced, mixed and got Mastered by Lizer from Wasafi Records Tanzania....The Video was shot in Tanzania by Director Nicorux from South Africa, on the 10th of April

TAARIFA YA MKUU WA MKOA KUHUSU HATUA ZINAZOENDELEA KUCHUKULIWA NA SERIKALI KUKABILIANA NA JANGA LA TETEMEKO LA ARDHI KAGERASEPTEMBA 17, 2016.

Ndugu Waandishi wa Habari, Kama mnavyojua Mkoa wetu wa Kagera ulipatwa na janga la tetemeko la ardhi tarehe 10.09.2016, kutokana na janga hilo Serikali kwa ikishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na wananchi tulichukua hatua za haraka ili kukabiliana na janga hilo, na leo nimewaiteni ili niwape taarifa tulizochukua mpaka sasa ili kunusuru wahanga waliokumbwa na janga hilo katika mkoa wetu.Ndugu Waandishi wa Habari, Mara baada ya tetemeko hilo kutokea, kwenye mkoa mzima wananchi waliojeruhiwa ni 440 na kati ya majeruhi hao 253 walifika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, pia majeruhi 151 walilazwa ambapo majeruhi 113 tayari wametibiwa na kuruhusiwa. Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wamebaki majeruhi 38 na kati ya hao majeruhi 23 walihitaji huduma za upasuaji na tayari wote wameishafanyiwa upasuaji huo na wanaendelea vizuri.Aidha, majeruhi 187 walifika katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya katika Mkoa wa Kagera na walitibiwa na kuruhusiwa na kufikia jumla ya majeruhi ambao walitibiwa na kuruhusiwa 412 kati ya 440. Vifo vilivyosababishwa na janga hilo ni 17 hadi kufikia siku ya leo.Ndugu Waandishi wa Habari, Tetemeko la ardhi mkoani Kagera hadi sasa limesababisha nyumba 2,063 kuanguka, Nyumba zenye uharibifu hatarishi 14,081. Nyumba zenye uharibifu mdogo 9,471. Aidha, wananchi walioathirika na wanahitaji misaada ili kurudi katika mfumo wa kawaida wa maisha yao ni 126,315Ndugu Waandishi wa Habari, Kufuatia madhara hayo yaliyojitokeza mahitaji mablimbali ya kibinadamu ya muda mfupi na muda mrefu yanahitajika. Mahitajihayo ni madawa na vifaa tiba, Chakula, Vifaa vya Ujenzi kama simenti, misumari, mabati na mbao.Hadi kufikia sasa Kamati ya maafa ya Mkoa wa Kagera tayari imepokea msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwa ni Madawa na vifaa tiba, Chakula, (Matrubali, mahema mashuka na mablanketi), vifaa vya ujenzi kama mbao, misumari, mabati na simenti vyenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni 431,715,800/=Ndugu Waandishi wa Habari, Kwa upande wa dawa na vifaa tiba wadau mbalimbali pamoja na Serikali wameweza kuchangia dawa na vifaa tiba vya kutosha hadi sasa hakuna upungufu wa dawa na vifaa tiba katika hospitali zetu.Aidha kwa mahitaji ya haraka tayari Kamati ya mkoa imegawa chakula kwa wahanga katika mkoa mzima kama ifuatavyo: unga wa sembe kilo 3750, mchele kilo 1850, sukari tani 6.5, maharage kilo 3470, bisukuti katoni 2600, na maji ya kunywa katoni 615. Pia wahanga wamegawiwa mahitaji muhimu kama mablanketi 480 mahema 119 na matrubali 320. Huo ulikuwa ugawaji wa mahitaji wa awali na kamati zinaendelea kugawa mahitaji hayo katika maeneo yaliyoathirika na yataendelea kugawiwa kadri tunavyopokea misaada ya mahitaji hayo.Ndugu Waandishi wa Habari, Napenda sasa kutoa taarifa ya michango mbalimbali ambayo tayari tumeipokea kutoka kwa wadau mbalimbali; Katika Harambee tuliyoifanya jana tarehe 16/09/2016 tuliweza kukusanya kiasi cha fedha taslimu pamoja na hundi 7,800,000/=, ahadi ya fedha na vifaa ni shilingi milioni 770,502,000/= kama wadau hawa wote watatoa michango yao jumla tutakuwa tumepata shilingi milioni 778,302,000/=
Kupitia Akaunti yetu iliyoko Benki ya CRDB inayojulikana kama “KAMATI YA MAAFA KAGERA CRDB BUKOBA” Akaunti Namba 0152225617300 tayari tumekusanya kiasi cha shilingi 623, 624,200/=. Aidha, baada ya Mhe, Waziri Mkuu kuzindua namba za simu za kuchangia maafa Kagera tayari wananchi wameanza kuchangia michango yao kupitia namba hizo ambazo ni (M.PESA 0768 196 669), (AIRTEL MONEY 0682 950 009), (TIGO PESA 0718 069 616).Ndugu Waandishi wa Habari, Napenda kuwashukuru wananchi na wadau mbalimbali wote wanaoendelea kujitoa kwa kuchangia maafa yaliyotupata katika Mkoa wetu wa Kagera pia natoa wito kwa kila Mwananchi, Mdau, Taasisi mbalimbali ambao hawajachangia kuendelea kuchangia kupitia akaunti ya benki na namba za simu zilizotajwa hapo juu kwani mahitaji bado ni makubwa sana.
Ndugu Waandishi wa Habari, Kabla ya kuhitimisha naomba kueleza mkakati wa Kamati yangu tunaondelea nao kuwa ni kugawa mahitaji mbalimbali kwa wahanga kadri tunavyoupokea. Pia wajumbe wote wa Kamati wamegawanywa katika maeneo mbalimbali ya mkoa yaliyopatwa na majanga ili kusimamia zoezi la kugawa mahitaji na kuhakikisha hakuna mwananchi aliyeathirika na janga la tetemeko ameachwa bila kusaidiwa.
Ndugu Waandishi wa Habari, Mwisho napenda kuwashukuru Waandishi wote wa Habari pamoja na vyombo vyao vya habari kwa kufanya kazi yao kwa ushirikiano mkubwa na Kamati yangu kwa kuwafikishia habari wananchi habari muhimu kuhusu janga lililotupata mkoa wetu.
MWISHO

Tamimu Omurungi na wimbo maalumu wa Tetemeko



Msanii Tamimu Omurungi aliamua kutumia nafasi yake kama msanii kwa kuwafariji wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera ambapo alifanikiwa kuurekodi siku1 baada ya tetemeko kwa producer Mpoki wa Fungu Records iliyopo mjini Bukoba. Pia wimbo huo umefaniwa video yenye animation za picha ya matukio ya tetemeko.

Pakua hapa Audio
Tamimu Omurungi_Tetemeko Kagera


Video

Tamimu Omurungi