Thursday, March 22, 2018

GoGoGo _ Cheza Kizamburi

Tamimu Omurungi Ft. Kamdingi Flani _ Akamotoka



Msanii mkali anayekuja kwa kasi kutoka mkoa wa Kagera Tamimu Omurungi ameachia ngoma yake mpya aliyoipa jina la 'Akamotoka' ambapo ndani yake kuna mchanganyiko wa lugha ya Kiswahili na kilugha cha Kihaya. Msanii huyo kwa kushirikiana na msanii mwenzake Kamdingi Flani wameweza kuachia audio na video za wimbo huo zinazofanya vyema kwenye vituo mbalimbali vya Redio na TV kanda ya ziwa na kupokewa vizuri na mashabiki wao. Kwa sasa video hiyo inapatikana You Tube, bofya kwenye link uitazame.


Friday, October 7, 2016

HISTORIA FUPI YA SCORPION MTOA MACHO


Alivyokuwa mdogo alikataa kusoma, mzazi alishafariki siku nyingi na alikuwa akilelewa na mama yake mdogo maeneo ya Yombo buza.

Alishawahi kufungwa jela japo haijajulikana alikosa nini, na jina lake kamili ni Salum Njwope na jina hilo nila babu yake. Yeye ni mwenyeji wa mkoa wa Shinyanga. Kwa mujibu wa mama yake mdogo anasema Scorpio alipokua akitoka nyumbani usiku saa mbili anamuaga mama yake mdogo huyo kuwa anakwenda kwenye kazi ya ubaunsa katika club kumbe mwenzie alikuwa anaenda Buguruni kuibia watu mpaka asubuhi ndio anarudi nyumbani.

Pia scorpion ashawahi kushiriki katika shindano lililojulikana kama Dume Challenge kama miaka mitatu iliyopita na aliibuka mshindi. Napia alianza mafunzo ya kucheza caret tangu akiwa mdogo sana napia ni mtu mwenye nguvu za kuzaliwa nazo.

Kuna kipindi aliondoka nyumbani kwao kwa muda mrefu mama yake mdogo anadai alikuwa hajui yuko wapi mpaka baadae aliporudi mwenyewe nyumbani.

Amekamatwa na Polisi baada ya kutuhumiwa kumjeruhi mkazi mmoja wa Dar es Salaam eneo la Buguruni kwa kumng’oa macho katika kitendo kilichoelezwa kuwa ni wizi wa fedha.

Salum Mrisho kijana aliyetolewa macho akiongea na vyombo vya habari, pembeni yake RC Makonda